Rais wa awamu ya nne wa UHURU KENYATTA
MGOMBEA wa
Urais nchini Kenya kwa tiketi ya muungano wa Chama cha CORD Raila Amolo Odinga
amekubali kushindwa katika kesi ya kupinga matokeo aliyofungua katika Mahakama
ya Juu nchini humo. Kenya Uhuru Kenyatta,
(kushoto) akijadiri jaambo na mpinzani wake Raila Odinga
Nairobi,Kenya
Akihutubia
taifa hilo muda mfupi uliopita,Odinga alisema kwamba anakubalina na hukumu hiyo
iliyosomwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga.
"Nimekubalina
na matokeo hayo kwa sababu yakuheshimu Katiba ya Kenya ambayo inasema matokeo
ya urais yapingwe katika Mahakama hiyo na maamuzi yatakayotolewa na Mahakama
ndiyo ya mwisho"alisema Odiga.
Alisema,
"Nilikwenda mahakamani kwa maslahi ya wakenya, hivyo natangaza rasmi
kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na kuitakia amani serikali iliyoko
madarakani,nitashikiana nao katika kujenga nchi yetu".
Odinga
ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu
Willy Mutunga kutoa hukumu ya kesi hiyo na kusema kwamba mahakama imekubali kwa
kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa huru na uwazi na kumfanya Kenyatta na
mgombea mwenza wake William Ruto kuchaguliwa kihalali.
No comments:
Post a Comment